LEARNING MANAGEMENT SYSTEM
KARIBU SANA IDF SCHOOLS
Ndugu Mzazi / Mlezi / Mwalimu / Mwanafunzi
Hii ni tovuti inayohusu mambo ya Kitaaluma katika Shule au Vituo vya Kielimu. Tovuti hii inarahisisha upatikanaji wa masomo ya shule za Chekechea, Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo kwa kutumia Mitaala ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Tanzania kupitia MTANDAO (ONLINE LEARNING).
IDFSCHOOLS ni mjumuiko wa shule au vituo vyote vya elimu vinavyoendeshwa au kusimamiwa na taasisi ya IDF (Islamic Development Foundation).
Vituo vinavyosimamiwa na IDF vinaanzia ngazi ya shule za Chekechea, Awali, Msingi, Sekondari mpaka Vyuo.
UNAWEZA KUFANYA NINI IDFSCHOOLS.ORG ?
- Mzazi/Mlezi: Kufatilia Usomaji wa Mwanafunzi, Kuona Kazi na Matokeo ya Mwanafunzi, Kuuliza, n.k
- Mwalimu: Kuandaa Somo/Kipindi, Kufundisha, Kusahihisha, Kutoa Maswali/Kazi (Homework), Kuona Matokeo, n.k
- Mwanafunzi: Kusoma, Kuuliza, Kujibu, Kufanya Maswali / Mitihani, Kupitia Past Paper, Kujipima Kasi ya Kujibu Maswali, n.k
MALENGO YA SHULE
- MWANAFUNZI AHIFADHI QUR’AN JUZUU MOJA (1) KILA MWAKA.
- (a) Kila Mwanafunzi Apate Ufaulu wa Daraja la Kwanza, la Pili au la Tatu (Division I, II, au III) (b) Kila Mwanafunzi Apate Ufaulu wa Somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK) kwa ALAMA ‘A’ au ‘B’
- Mwanafunzi na Mwalimu kuwa na Maadili na Hamasa au Ari ya Kuitumikia Dini na Jamii kwa Ujumla